Jumapili 12 Aprili 2026 - 16:30
Tunasisitiza haki ya Lebanon na Muqawama wa Kiislamu katika kutoa jibu halali kwa uvamizi wa wazi

Hawza/ Ofisi ya Kisiasa ya Ansarullah ya Yemen imelaani uhalifu wa kutisha uliotekelezwa na utawala wa adui Muisraeli dhidi ya taifa la Lebanon, uliosababisha mamia ya mashahidi na majeruhi.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ofisi ya Kisiasa ya Ansarullah ya Yemen imesisitiza haki ya Lebanon na muqawama wa Kiislamu katika kutoa jibu halali kwa uvamizi huu wa wazi, na ikawataka watu na Umma wa Kiislamu pamoja na watu huru duniani waoneshe mshikamano mpana na taifa la Lebanon mbele ya ujeuri wa Kizayuni.

Ofisi ya Kisiasa ya Ansarullah katika tamko lake, ililaani uhalifu wa kutisha uliotekelezwa na utawala wa adui Muisraeli dhidi ya taifa la Lebanon, uliosababisha mamia ya mashahidi na majeruhi, na ikaeleza uvamizi huu kuwa ni kielelezo cha kiwango cha unyama, uhalifu na chuki ya Kizayuni dhidi ya Lebanon na Umma kwa ujumla.

Tamko hilo lilieleza kuwa utawala mhalifu wa Kizayuni, ambao mikono yake imechafuliwa na damu ya watoto na wanawake huko Ghaza na katika mataifa mengine ya Umma, umeshindwa dhahiru katika vita hivi, na sasa kupitia uhalifu huu unafanana na mtu anaeghariki anayeshika kila tawi ili kujinusuru, baada ya kuwa na yakini kwamba amepata pigo kubwa yeye pamoja na Marekani kutoka kwa mhimili wa jihadi na muqawama.

Tamko hilo lilifafanua kwamba; adui Muisraeli anajaribu kufidia hasara na kushindwa kwake katika vita kwa kutekeleza uhalifu zaidi wa kinyama dhidi ya mataifa ya Umma.

Ansarullah pia ilitaja uhalifu wa adui Muisraeli dhidi ya taifa la Lebanon kuwa ni “uhalifu wa wazi wa mauaji ya kimbari (genocide)” unaotokea mbele ya macho ya Umoja wa Mataifa na taasisi za kimataifa za haki za binadamu.

Katika tamko hilo ilisisitizwa kwamba; uhalifu huu hautadhoofisha kamwe azma ya taifa la Lebanon na mujahidina wake mashujaa, bali utaongeza nguvu, uthabiti na dhamira yao ya kuendelea na njia ya jihadi na muqawama, na unathibitisha usahihi wa chaguo la jihadi na muqawama, huku ukisisitiza kwamba chaguo la maridhiano na sera ya kutoa mapendeleo humfanya adui kuwa na ujasiri zaidi katika uasi, uhalifu na unyama.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha